Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi auawa akitafuta kuni

E3cb6d8e465799298358555a61116c4b Mwanafunzi auawa akitafuta kuni

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWANAFUNZI wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kivukoni na mkazi wa mtaa wa Nyantorotoro “B” mkoani Geita, Naomi James anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za mwili wake katika shamba la miti alipokuwa na wenzake watatu wakichanja kuni.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo limetokea Januari 18 mwaka huu na wanamshikilia Said Shaban (39) kwa tuhuma za kumuua Naomi James (17).

Kamanda Mwaibambe alisema mwanafunzi huyo alikuwa kidato cha pili katika shule ya sekondari Kivukoni na mwili wake umepatikana katika shamba la miti alipokuwa akitafuta kuni na wenzake wawili wa darasa la saba waliofanikiwa kukimbia baada ya mtuhumiwa huyo kuwakimbiza na kumkamata Naomi na kumshambulia.

Akizungumzia tukio hilo baba mzazi James Bulabo na ndugu wa mtoto huyo Deusdedit Yegela walieleza kusikitishwa na kitendo cha kuuawa mtoto wao na kuziomba mamlaka husika likiwemo jeshi la polisi kumfikisha mtuhumiwa huyo mahakamani haraka kujibu tuhuma hizo ili haki iweze kupatikana.

Polisi jamii na wajumbe wa serikali ya mtaa huo Martin John, Sweetbet Elikana na Joyce Nkilijua walisema walipata taarifa kutoka kwa familia ya marehemu kuwa mtoto wao haonekani nyumbani ndipo walipoanza kufanya uchunguzi na kupata taarifa kutoka kwa wanafunzi waliokuwa naye porini.

Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyantorotoro “B”, Nyerere Katoyo aliwataka wamiliki wa mashamba ya miti katika eneo hilo kuhakikisha wanayafanyia usafi kila mara ili kundoa changamoto za watu kutumia vichaka hivyo kufanya vitendo vya uhalifu na kutolea mfano tukio hilo.

Baadhi ya wananchi wa mtaa huo Amon Busumba, Magreth Daud na Ashura Joseph wamelaani kutokea kwa tukio hilo na kuiomba serikali kuchukua hatua kali dhidi ya mtuhumiwa wa tukio hilo ili iwe fundisho kwa watu wengine .

Chanzo: habarileo.co.tz