Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi atuhumiwa kuua mwenzake chuoni

BLASIUS Mwanafunzi atuhumiwa kuua mwenzake chuoni

Fri, 26 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAFUNZI wa Chuo cha Utumishi Kange, jijini hapa anadaiwa kumuua mwanafunzi mwenzake kwa kumchoma kisu baada ya kumkuta kwenye chumba cha rafiki yake wa kike.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi, Blasius Chatanda, alithibitisha jana kwa njia ya simu kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa palitokea ugomvi baina ya wanafunzi wa kiume.

Ugomvi huo ulizuka juzi, baada ya kukutana kwenye chumba cha msichana huyo, huku kila mmoja akiona kuwa ana haki ya kummiliki msichana huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda Chatanda, aliyefariki dunia katika tukio hilo ni Hussein Daud, ambaye anadaiwa alichomwa kisu na Waziri Ramadhan.

Alifafanua kuwa Daudi alikutwa ndani ya binti huyo.

“Huyu Hussein Daudi aliuawa kwa kuchomwa kisu na mtu anayedaiwa kuwa ni Waziri Ramadhan kwa sababu ya wivu wa mapenzi,” alisema na kuongeza:

"Walikutana kwenye chumba cha binti huyo, ndipo walipoanza kugombana wakidhani kuwa kila mmoja anayo haki ya kummiliki."

"Sasa katika ugomvi huo wakiwa chumbani kwa msichana huyo, Waziri Ramadhan alichukua kisu na kumchoma Daud na kusababisha kifo chake papo hapo."

Aidha, Kamanda Chatanda alisema tukio hilo haliwezi kufananishwa na tukio la fumanizi, na kwamba vijana hao wote wawili wamekatisha ndoto zao.

Kutokana na tukio hilo, Kamanda Chatanda aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo kwa kuwa hicho ndicho kilichowapeleka hapo.

Kamanda huyo alisema wanamshikilia binti huyo, huku mtuhumiwa akidaiwa kukimbia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live