Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi anaswa akiwa na shisha darasani

Mwanafunzi Anaswa Akiwa Na Shisha Darasani Mwanafunzi anaswa akiwa na shisha darasani

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya Mjini Unguja ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Rashid Simai Msaraka amepiga marufuku ya Shisha pamoja na matumizi ya simu kwa wanafunzi katika skuli zote za Wilaya hiyo

Dc Msaraka amepiga marufuku hiyo wakati alipoendesha zoezi la kushtukiza la kuwakagua wanafunzi katika skuli ya sekondari Forodhani ikiwa ni muendelezo wa ziara hizo kwa skuli mbalimbali za wilaya ya Mjini

Msaraka amesema katika operesheni hiyo wamekamata Simu, shisha na vitu vyengine ambavyo havitakiwi kutumika na wanafunzi

Amesema marufuku hiyo itaendana na ufatiliaji wa kushtukiza mara kwa mara katika skuli zote za wilaya yake ambapo amewatahadharisha wanafunzi kutii agizo hilo

Kaimu Kamanda wa Polisi wilaya ya Mjini SP Edward Lusekelo amesema wanafunzi watakaobainika kutenda makosa hayo ikiwemo kukamatwa na madawa ya kulevya na shisha watafikishwa kituoni na kuwaita wazazi wao kwa mahojiano zaidi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live