Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi amuua mwenzake naye ajikata tumbo

IMG 20220909 WA0011 Mwanafunzi amuua mwenzake naye ajikata tumbo

Fri, 9 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Winfrida Michael (24) mwanafunzi wa Chuo cha St John amefariki baada ya kuchomwa kisu na mpenzi wake Julias Gervas (26) ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho sababu ikitajwa kuwa wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,  Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa  baada ya Julius kufanya mauaji hayo alijaribu kujiua kwa kujikata tumbo na sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Dodoma.

Ofisa muuguzi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma,  Ester Ngoloki amesema Septemba 7, 2022 walimpokea Julias akiwa na jeraha la kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumboni.

Amesema walimpokea Ester akiwa amefariki na mwili wake ukiwa na majeraha ya kitu chenye ncha kali.

“Majeruhi yupo hospitali akiendelea kupatiwa matibabu na anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji na mwili wa Winjfrida umechukuliwa na ndugu kwa ajili ya taratibu za familia,” amesema.

Chanzo: Mwananchi