Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi amchoma kisu mwenzie kisa kofia

KITCHEN Mwanafunzi amchoma kisu mwenzie kisa kofia

Mon, 17 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyerere, Tanu Warioba leo Jumatatu Mei 17 amethibitisha kumpokea majeruhi huyo na kulazimika kumshona na mpaka sasa amelazwa hospitalini hapo.

"Amelezwa wodi ya wanaume ana nafuu, nilipouliza chanzo akadai ni kofia yake aliyokuwa nayo mwenzake baada ya kumdai kukaibuka ugomvi na ndipo alipomchoma kisu tumboni," amesema Warioba.

Kwa upande wake, Ofisa mtendaji wa Kijiji cha Rung'abure, Esther Nyarhobi, amesema majeruhi alikuwa anamdai mwanafunzi mwenzake kofia na walipokutana Mei 16, 2021 mchana kukatokea mzozo ndipo mtuhumiwa akamchoma kisu kisha kukimbia.

"alipochomwa kisu alianguka chini akipiga kelele, mtuhumiwa akakimbia na watu wakajotokeza kumpa msaada na kumkimbiza hHospitali kwa matibabu. Tukio hilo limetushangaza hawa ni majirani na wanasoma darasa moja kofia kuzua balaa zito hivi inatuchanganya," amesema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema Polisi wanaendelea kumsaka mtuhumiwa ili akamatwe na kuomba wananchi kuwapa ushirikiano.

Chanzo: ippmedia.com