Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi ajinyonga baada ya kuzuiwa kujihusisha na mapenzi

Mwanafunzi Ajinyonga Baada Ya Kuzuiwa Kujihusisha Na Mapenzi Mwanafunzi ajinyonga baada ya kuzuiwa kujihusisha na mapenzi

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lasmin Kondo mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Masaki, wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, amekutwa akiwa amejinyonga baada ya kukatazwa na wazazi wake kutojihusisha na mapenzi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa jeshi la polisi mkoani Pwani, ACP -Pius Lutumo anasema, ni matukio mawili ya watu wawili kupoteza maisha katika matukio mawili tofauti yaliyotokeza wilayani Kisarawe.

Akielezea tukio la kwanza, alieleza mwanafunzi huyo amejinyonga baada ya kugombezwa na wazazi wake kutojihusisha na matukio ya mapenzi kufuatia kukutwa na barua aliyokua amemuandikia mpenzi wake.

Katika hatua nyingine,kamanda LUTUMO ameeleza kuwa PILI MANG’OTA ambae ni mkulima wa mboga mboga na mkazi wa Sanze Kisarawe ,amekutwa amefariki dunia.

“Mwanamke huyu aliaga kwenda Visegese kuchukua mboga lakini hakurudi tena hadi umauti ulipomkuta na kukutwa vichakani akiwa amefukiwa akiwa amefariki,”alifafanua Lutumo.

Kufuatia kifo cha mwanamke huyo, jeshi hilo linamsaka mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la ABDALLAH ambae ni mume wa marehemu kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mkewe.

Jeshi hilo pialimeendelea na msako wake na kufanikia kubaini matukio mengine ya uhalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live