Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi ahukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwa unyanyasaji wa kijinsia

23 1 660x400 Mwanafunzi ahukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwa unyanyasaji wa kijinsia

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Ahmed Bassem Zaki (22) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kukutwa na Hatia ya kuwanyanyasa kijinsia Wanawake wawili kupitia Mitandao ya Kijamii.

Mahakama inayoshughulikia Uhalifu wa Kimtandao, ilimkuta Mwanafunzi huyo na hatia ya kutuma picha na jumbe zenye maudhui ya ngono kwenye simu za Wanawake.

Unyanyasaji wa Kijinsia ni kosa kisheria nchini humo tangu mwaka 2014, na mashtaka dhidi ya Zaki yalichochea kwa kiasi kikubwa Kampeni ya MeToo ambapo Wanawake walijitokeza kuripoti matukio hayo.

Kesi hiyo ilipata umaarufu Misri ambapo Wanaharakati wa Haki za Wanawake wanadai Unyanyasaji wa Kijinsia ni janga kubwa ambalo halipewi uzito.

HOTEL YA SUGU KUBOMOLEWA, RAIS MAGUFULI AZUIA “MSIBOMOE HOTEL SUGU, MSILETE SIASA”

Chanzo: millardayo.com