Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi afariki akiigiza kujinyonga

121597892 988452578320675 4768364736722081012 N.png Mwanafunzi afariki akiigiza kujinyonga

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Mwanafunzi wa Darasa la tatu shule ya Msingi Ikelu Makambako mkoani Njombe, Claud Frolence (9) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kikoi akiwa anacheza na wenzake shambani.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Hamisi Issa amesema mwanafunzi huyo alikwenda shambani na wazazi wake na wadogo zake watatu akiwa huko walianza kucheza na wadogo zake na baadae kuchukua kikoi na kuanza kucheza michezo ya kujaribu namna ya kujinyonga.

Aidha kamanda Kamanda Issa amewataka wazazi kuwa makini na malezi ya watoto wao kwani malezi ya Watoto ni pamoja na kuangalia aina ya michezo wanayoicheza na katika mazingira  yanayofaa.

JAJI WARIOBA “SOKOINE HAKUJILIMBIKIZIA MALI, ALIPEWA MADARAKA AKAKATAA NI WACHACHE SANA”

Chanzo: millardayo.com