Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi adaiwa kuuawa kwa kitu cha ncha kali

20558 PIC+MWANAFUNZI TanzaniaWeb

Wed, 3 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Jumbi, Sabra Ussi Khamis amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mtu anayedaiwa kuwa mgonjwa wa akili.

Tukio la kuuawa kwa binti huyo limetokea jana Oktoba 2, 2018 majira ya saa mbili usiku wakati Sabra alipokua akiuza duka nyumbani kwao na ghafla alitokea kijana huyo anayesadikiwa kuwa mgonjwa wa akili Hafidh Mkubwa Suleiman (21) na kumchoma na kitu tumboni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Thobias Sedeyoka amesema ni kweli tukio hilo limetokea na wanaendelea na uchunguzi kubaini taarifa zaidi.

Amesema taarifa za awali zinadai kuwa anayetuhumiwa kufanya tendo hilo ni mgonjwa wa akili lakini wao kama jeshi la polisi wanahitaji kufanya uchunguzi wa kina kubaini ukweli huo.

Sedeyoka ametoa wito kwa jamii kutowaacha watu wenye ulemavu wakiendelea kuzunguka mitaani iwapo watagundua wamekua wakihatarisha maisha ya raia wengine.

Akizungumzia tukio hilo, Iddi Abdalla Haji amesema mara baada ya binti huyo kuchomwa na kitu cha ncha kali alianguka ghafla huku akipiga kelele kuashiria kuomba msaada wakati akiwa amejishika tumboni.

Chanzo: mwananchi.co.tz