Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi UDSM akamatwa kwa madai ya kutoa taarifa za uongo za corona

102154 Pic+udsm Mwanafunzi UDSM akamatwa kwa madai ya kutoa taarifa za uongo za corona

Sat, 11 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga. Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dare es Salaam mwaka wa tatu katika  kitivo cha Kiswahili kwa kosa la kusambaza kwenye mitandao ya kijamii taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa corona.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Mariamu Jumanne Sanane (23) ambaye alikamatwa Aprili 9, mwaka huu usiku katika  eneo la mtaa wa Tabora katika Mgodi wa Almasi wa Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Kamanda Magiligimba amesema mnamo  Machi 26 mwaka huu askari wa kikosi kazi cha mitandao ya kijamii walifanikiwa kuona ujumbe kwenye mtandao wa whatsap uliotumwa na mtuhumiwa ukisomeka, “…Mpk ss Tanzania ina wagonjwa wapatao takriban 230 wa COVID 19 na waliofariki ni 04.”

Mtuhumiwa baada ya kupekuliwa alikutwa na simu iliyotumika kutuma ujumbe huo ambapo tayari amehojiwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo mitandaoni na kutoa takwimu za uongo.

“Nitoe wito kwa wananchi wote kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii na waache kupotosha watu kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai watachukuliwa hatua Kali za kisheria,” alisisitiza Magiligimba

Chanzo: mwananchi.co.tz