Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanachuo amuua mwanaye na kumla nyama

Fisi Mauaji?fit=613%2C356&ssl=1 Mwanachuo amuua mwanaye na kumla nyama

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Olivia Naseren (24) mkazi wa Kitengela, Kaunti ya Kajiado, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoa visu binti yake Glory Njeri (2) kisha kula sehemu ya viungo vya mwili wake kufuatia mgogoro wa kimapenzi uliosababisha kuvunjika kwa uhusiano kati yake na baba wa mtoto.

Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi, mwanamke huyo alikuwa amejifungia ndani akicheza na mwanaye kabla majirani hawajasikia sauti tata zilizoashiria mambo kutokuwa sawa ndani ya nyumba hiyo.

Sehemu nyingine ya ripoti ya polisi inadai mwanamke huyo ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Kenya akisoma masomo ya biashara, alianza kuvunja kwanza TV, kisha kumchoma visu mwanaye ambaye baada ya kufariki alikula pia sehemu ya utumbo na figo zake.

Hadi majirani wanafanikiwa kuvunja nyumba na kuingia ndani, tayari mtoto huyo alikuwa kachomwa zaidi ya visu 100, akiwa amekatwa shingo na viungo vya mwili wake kunyofolewa, mwili wake unahifadhiwa kwenye Mochwari za moja ya hospitali iliyopo Kaunti ya Kitengela kwa uchunguzi wa kitabibu.

Mashuhuda wamedai kuwa, mama huyo ambaye pia ni mwalimu mwenye alikuwa uchi wa mnyama huku akianguka na kuzirai kando ya maiti ya bintiye wakati chumba kizima kikitapakaa damu.

Polisi pia walipata kisu kilichotumika kumuua mtoto huyo ambapo mshukiwa alitiwa nguvuni na kupelekwa hospitali ya kaunti ndogo ya Kitengela huku maiti ya mtoto huyo ilihifadhiwa katika mochari ya hospitali hiyo.

Jumatatu alasiri Olivia alipata nafuu na kupelekwa kuzuiliwa katika kituo cha polisi Kitengela kuhojiwa. Mshukiwa huyo alifichua kwamba alitekeleza uhalifu huo kwa sababu ya kujichukia.

“Ninajichukia mwenyewe. Sijipendi ndio maana niliua mtoto wangu. Nimepitia magumu na huyu mtoto.”

Pia aliongeza kusema awali alitaka kujiua mwenyewe lakini akabadilisha mawazo. Kuna wakati Olivia alinyamaza kabisa bila kuzugumza lakini akiwa amezama kwa mawazo.

Afisa wa uchunguzi wa Jinai Kitengela Bw Benson Mutia alisema kwamba uchunguzi umeanza kufanyika na punde tu utakapokamilika Olivia atapelekwa kortini. Mutia alisema Olivia hajahojiwa kwa vile ameruhusiwa kutoka hospitali Jumatatu alasiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live