Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu wa dini mbaroni kwa kulawiti watoto

Mwalimu Pic Data Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ACP, Ally Makame

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limemkamata mwalimu wa mafundisho ya dini katika Kanisa la Katoliki Mpanda Mjini, Joseph John (27) akituhumiwa kuwalawiti watoto wanne.   Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Februari 10, 2022 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ACP, Ally Makame amesema mtuhumiwa ametenda kosa hilo maeneo tofauti.

Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Februari 03, 2022 akiwalaghai watoto hao wamsindikize kwenda kufanya shughuli za biashara sehemu tofauti.

"Alikuwa anawabeba kwenye pikipiki yake baada ya kumaliza vipindi vyao vya masomo ya kidini kisha kuwafanyia ukatili huo," amesema Makame.

"Baada ya kumkamata tulimhoji akakiri kufanya hivyo, lakini baadhi ya watoto tuliowahoji wamekubali kufanyiwa," amesema.

Kamanda Makame amesema upelelezi wa shauri lake umekamilika na kwamba mtuhumiwa amefikishwa mahakamani.

Advertisement Kutokana na hali hiyo ametoa rai kwa viongozi wa taasisi za kidini kutojihusisha na uovu kwa kigezo cha kutumia imani zao.

"Wazazi walimuamini kuwa yeye ni mwalimu nisiaitize tabia hiyo ikome ni ukiukwaji wa sheria na inaathari kubwa kwa watoto," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live