Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu wa Madrasa atuhumiwa kulawiti wanafunzi 10

Mwalimu Wa Madrasa Atuhumiwa Kulawiti Wanafunzi 10 Mwalimu wa Madrasa atuhumiwa kulawiti wanafunzi 10

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: Eatv

Mwalimu wa Madrasa katika msikiti wa Mohamed Shunu uliopo Mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama, aliyefahamika kwa jina moja la Faidhi anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kuwalawiti wanafunzi 10 wa madrasa kwa nyakati tofauti kwa kuwarubuni kuwapa Sh 1000 na Sh 500

Akizungumza Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha mwalimu huyo kukamatwa ambapo baada ya kufanya vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto kuanzia umri wa miaka sita hadi 11 alitoroka  na kukimbilia Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma na walipofuatilia wamemkamata na amerudishwa Kahama kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kamanda Magomi amesema Mwalimu huyo aliwarubuni watoto hao kwa kuwapa Sh 1000 na wengine Sh 500 kisha kuwafanyia kitendo hicho ambacho ni kinyume na maadili na kuwataka wazazi na walezi kuwafichuwa watu wanaowafanyia vitendo vya kikatili watoto wao badala ya kuwaficha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Shunu Manispaa ya Kahama, Joseph Kaliwa amesema alipata taarifa kutoka kwa wananchi siku ya Ijumaa juu ya kulawitiwa watoto na kushirikisha viongozi wengine ndipo walipoanza kufuatilia na kuandaa kikao cha wazazi ili kupata maelezo ya kina kisha watoto wote walikwenda kufanyiwa uchunguzi hospitali ya Rufaa Kahama na kubaini wameingiliwa.  

Chanzo: Eatv