Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu mstaafu ashikiliwa kwa kufuja Sh198 milioni

Mwalimu Pc Data Mwalimu mstaafu ashikiliwa kwa kufuja Sh198 milioni

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Taasisi ya Kizuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imemkamata na kumfikisha mahakamani mwalimu Raphael Munada kosa la uhujumu uchumi.

Munada ambaye alikuwa Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) anashikiriwa kwa kosa la ubadhirifu wa Sh198 milioni ambazo zilipangwa kununua mabati kwa ajili ya walimu wastaafu mwaka 2017.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amekiri kushikiliwa kwa Munada akisema wameshamfikisha mahakamani.

"Siwezi kuwa msemaji zaidi sababu tumeshamfikisha mahakamani, lakini tulimkamata baada ya uchunguzi wetu kuona anahusika na upotevu wa karibu Sh198 milioni," amesema.

Munada katika uongozi wake ndani ya Jiji la Dodoma aliingia katika mgogoro kati yake na aliyekuwa Mwenyekiti wa CWT wilaya hiyo, Samson Mkotya na mjumbe wa kamati ya Utendaji walipomtuhumu kuwa anafuja mali za chama.

Ofisa habari wa CWT, Bathlomeo Chilwa amesema taarifa hizo anazo lakini mhusika sio mtumishi wao kwa hiyo hawezi kulizungumzia jambo hilo.

Chanzo: mwananchidigital