Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu mkuu adaiwa kujiua kwa kunywa sumu

Mwalimu Mkuu Adaiwa Kujiua Kwa Kunywa Sumu Mwalimu mkuu adaiwa kujiua kwa kunywa sumu

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: Malunde

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtanila iliyopo kijiji cha Igangwe wilayani Chunya mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kudaiwa kunywa kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni sumu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga tukio hilo limetokea kijijini Igangwe Septemba 14 mwaka huu saa moja na nusu asubuhi.

Kamanda Kuzaga alimtaja Mwalimu Mkuu huyo kuwa ni Magwira Nkuta(41) mkazi katika kijiji cha Igangwe wilayani Chunya.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo kwani inadaiwa kuwa kabla ya ujio wa mbio za Mwenge wa Uhuru, marehemu alikabidhiwa fedha na ofisi ya Takukuru kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kibao cha “KLABU YA TAKUKURU RAFIKI SHULENI” lakini pamoja na kutumiwa fedha hizo hakuweza kutengeneza kibao hicho hadi Mwenge wa Uhuru ulipofika shuleni hapo kwa ajili ya ufunguzi wa Klabu hiyo.

Chanzo: Malunde