Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu mbaroni kwa kutuma vitisho Halmashauri

Mbaroni Mwalimu mbaroni kwa kutuma vitisho Halmashauri

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Hanihani katika kata ya Igunga mjini, Paul Msabila amepandishwa kizimbani akidaiwa kutishia kwa njia ya simu.

Katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga, Mwendesha Mashitaka wa Polisi Wilaya ya Igunga, Rammy Magoha alidai mbele ya hakimu wa Wilaya ya Igunga, Edda Kahindi mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi 11 mwaka huu saa nne asubuhi katika Kata ya Igunga wilayani humo katika Mkoa wa Tabora.

Magoha alidai kuwa mshitakiwa Msabila alitumia simu janja ambayo ni mali yake kutuma ujumbe kwenye kundi katika mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwa watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.

Aliwataja watumishi hao ni Joseph Sambo ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Igunga, Sophia Maziku, Mussa Abdallah Ofisa Utumishi Igunga, Dora Simba ambae ni Ofisa Elimu Shule za Msingi Wilaya ya Igunga na Loyce Matata.

Magoha alidai kuwa Msabila alifanya hivyo kwa lengo la kuwatishia maisha ikiwa kuwaogopesha na kuwasababishia usumbufu wa kisaikolojia.

Msabila alikana shitaka na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 30 mwaka huu. Mshitakiwa amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live