Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu kortini kwa kumuingilia mtoto miaka 11

Mwalimu Kingono Mwalimu kortini kwa kumuingilia mtoto miaka 11

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: mtanzania

Mwalimu wa kujitolea na mkazi wa Mwanamtoti Mbagala Dar es Salaam, Ally Said Kaule maarufu Sir Ally(26) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa kosa la kumuingilia kingono.

Akisomewa hati ya mashtaka leo Jumanne Oktoba 11, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Aziza Mbajo, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Grace Lwila amedai kuwa katika tarehe isiyojulikana Agosti, mwaka huu eneo la Mbagala Mwanamtoti mshtakiwa alimuingilia kingono mtoto wa miaka (11) jina linahifadhiwa.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo mbele ya mahakama na Mwendesha mashtaka amedai upelelezi umekamilika

Hakimu Mbajo amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakao saini bondi ya Sh milioni 3 kila mmoja.

Hata hivyo, mshtakiwa amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo namba 551 ya mwaka 2022 itatajwa tena Oktoba 25, mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Sir Ally ambaye ni Mwalimu wa kujitolea katika Shule ya Msingi Mbagala Kuu wilayani Temeke, Dar es Salaam katika tarehe isiyojulikana Agosti, mwaka huu alimuingilia kingono mtoto huyo.

Chanzo: mtanzania