Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu kizimbani kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake

94795 Wakili+pic Mwalimu kizimbani kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lindi. Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mahiwa mkoani Lindi,  John Ngalu amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Lindi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tano.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Februari 6, 2020 na mkuu wa mashtaka Mkoa wa Lindi, Juma Maige wakati akizungumza na Mwananchi.

Amesema mwalimu huyo alifikishwa mahakamani jana Jumatano baada ya kufunguliwa kesi namba 4/2020, anadaiwa kufanya kitendo hicho katika nyumba iliyopo karibu na shule hiyo.

Maige amesema Ngalu alikutwa na mwanafunzi wa shule hiyo wakiwa watupu.

Amebainisha kuwa vitendo vya namna hiyo kwa mwalimu huyo  na mwanafunzi  wake  ni vya muda, kwamba kesi hiyo iliahirishwa hadi Februari 13, 2020 na mwalimu huyo kurudishwa rumande.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz