Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu jela miaka 30 kwa kumlawiti mwanafunzi

NahakamaniipiicHHH Mwalimu jela miaka 30 kwa kumlawiti mwanafunzi

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma mkoani Mara, imemuhukumu kwenda jela miaka 30 mwalimu Idrisa Athumani (29) wa shule ya Msingi Kyawazaru iliyopo wilayani Butiama baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake

Hukumu hiyo imetolewa leo Septemba 16,2022 ikiwa ni siku mbili tu tangu mwalimu huyo  kuhukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Musoma  baada ya kupatikana na hatia ya  kulawiti mwanafunzi mwingine.

Akisoma hukumu hiyo leo, Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Erick Marley amesema kuwa mahakama hiyo imejiridhisha pasi  na shaka kuwa mwalimu huyo aliyeajiriwa Desemba mwaka 2020 na kuanza kazi shuleni hapo Januari, 2021  alitenda kosa hilo kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.

"Mahakama hii inakutia hatiani kutokana  na kosa uliloshtakiwa nalo na ili iwe mfano kwako wewe na wengine wenye tabia kama yako ukizingatia kuwa umekabidhiwa watoto ili kuwatunza na hili suala ni kinyume na tamaduni zetu, halitakiwi wala kuruhusiwa nakuhukumu kwenda jela miaka 30" amesema

Akisoma maelezo ya shtaka hilo, hakimu Marley amesema kuwa mwalimu huyo alishtakiwa Julai 20, 2022 kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake wa  darasa la sita mwenye umri wa miaka 12.

Amesema kuwa mwalimu alifanya kosa hilo kinyume cha kifungu namba 154 kifungu kidogo cha kwanza (a) na cha pili cha kanuni ya adhabu sura namba 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 na kufunguliwa kesi  namba 50 ya mwaka 2022.

Ameeleza kuwa mashahidi wanne walitoa ushahidi huo ambao bila shaka yoyote umemtia hatiani mwalimu huyo ambapo amesema kuwa miongoni mwa waliotoa ushahidi ni daktari na mwalimu mkuu msaidizi.

Wakili wa Serikali ambaye pia ni mwendesha mashtaka kiongozi, Jesse Temba, amedai Athumani alitenda kosa hilo katika kijiji cha Kyawazaru nyuma ya tenki la maji lililopo nusu kilomita kutoka shule ya msingi Kyawazaru.

" Tukio lilifanyika tarehe ambayo bado haujajulikana Mei mwaka huu majira ya saa nane mchana baada ya mshtakiwa kumuita mwanafunzi wake akiwa na nia ya kutenda kosa hili" amesema

Amesema kuwa siku ya tukio mwalimu huyo alimuita mwanafunzi huyo kisha kumtaka avue nguo agizo ambalo mwanafunzi huyo aligoma kutekeleza kisha mwalimu kumshika kwa nguvu na kumvua nguo kisha kumuinamisha na kutenda kosa hilo.

Alipotakiwa kujitetea mwalimu huyo ambaye ni mwalimu wa nidhamu shuleni kwake ameiomba mahakama hiyo kumpa adhabu ndogo kwani yeye ni baba wa familia mwenye mke mmoja na watoto wawili hivyo familia yake inamtegemea.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz