Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu jela miaka 20 kwa kumdhalilisha kingono mwanafunzi wa miaka 11

61827 NGONO+PIC

Mon, 10 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mwalimu wa Shule ya Msingi Uru iliyopo Kata ya Uru, Wilaya ya Moshi, Fidelis Matemu (60), amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kumdhalilisha kingono, mtoto wa miaka 11.

Hukumu hiyo ilitolewa jana Juni 7, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Pamela Mazengo, baada ya hakimu huyo kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka.

Awali, mawakili wa Serikali, Ignas Mwinuka na Grace Kabu walidai kuwa Aprili 26, 2018 huko kijiji cha Uru Njari, mshtakiwa alimdhalilisha mtoto huyo anayesoma darasa la sita Shule ya Msingi Msareni.

Ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi hao ulieleza kuwa siku hiyo, mtoto huyo alikuwa peke yake nyumbani na mshtakiwa alifika nyumbani hapo akitaka kununua sabuni.

Wakati mtoto huyo akiwa katika harakati za kumuuzia sabuni, mshtakiwa alimshika na kumuingiza kwenye chumba kimojawapo kilichopo ndani ya duka hilo na kuanza kumvua nguo na kuanza kumuingizia vidole sehemu za siri.

Katika purukushani hizo, mtoto huyo alipata upenyo wa kukimbia nje na kumuarifu shangazi yake na baadaye uongozi wa mtaa uliarifiwa na baadaye taarifa hizo zilifikishwa polisi ndipo mtuhumiwa akakamatwa.

Pia Soma

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mazengo alisema ushahidi dhidi ya mshtakiwa ulikuwa mzito na haukuacha shaka yoyote kuwa alitenda kitendo hicho hivyo atatumikia kifungo cha miaka 20 jela.

Chanzo: mwananchi.co.tz