Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu auawa, mdogo wake ajeruhiwa vibaya

Mauaji Nn.jpeg Mwalimu auawa, mdogo wake ajeruhiwa vibaya

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mara kwa tuhuma za kumuua Mwalimu Saidi Hamisi wa shule ya sekondari Masaba iliyopo Kijiji cha Nyasirori wilayani Butiama na kumjeruhi vibaya mdogo wa marehemu huku wakiwaibia simu za uwakala pamoja na kompyuta kompyuta mpakato moja.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Dismas Kisusi, amesema tukio hilo limetokea usiku wa Agosti 26 mwezi huu ambapo Mwalimu huyo alikuwa anatoka katika ofisi yake ya biashara.

Aidha Kamanda amesema kuwa uchunguzi uyakapo kamilika.watu hao watafikishwa mahakamani ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wengine ambao wamehusika katika kutenda kosa hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live