Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu auawa baada ya kukataa kununua pombe

98224 Pic+mwalimu Mwalimu auawa baada ya kukataa kununua pombe

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katavi. Mwalimu wa  Shule ya Msingi Mbugani kata ya Kakese,   Shauri Kiani  (35) amefariki  baada ya kupigwa na tofali kichwa kutokana na kukataa kumnunulia pombe anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Leo Ijumaa Machi 6, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea tukio, “limetokea Machi 3, 2020 saa 5 usiku eneo la  Mbugani. Mtuhumiwa ni  Omary Juma (30) mkazi wa Kakese. Kiani  alikimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi lakini alifariki wakati anapatiwa matibabu.”

Amesema polisi walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa anayeendelea kuhojiwa, kwamba muda wowote atafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, polisi wanamshikilia Nchemba Masunga (22) mkazi wa kijiji cha Mawiti anayedaiwa kumlawiti mtoto wa miaka 13 mkazi wa tarafa ya Mamba wilaya ya Mlele.

Kuzaga amesema tukio hilo lilitokea Machi 3, 2020 saa 6 usiku, “mtuhumiwa alijificha kwenye kichaka na mtoto huyo wakati akipita eneo hilo akitokea shambani, alimvamia na kumlawiti.”

Chanzo: mwananchi.co.tz