Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu atuhumiwa kufanya mapenz kitanda kimoja na wanafunzi wawili

69653 8f04c652 4cce 46de A324 B3da71af6ead 1 660x400 Mwalimu atuhumiwa kufanya mapenz kitanda kimoja na wanafunzi wawili

Thu, 13 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Salum Kalii, ameagiza Mwalimu Martin Mambosasa, wa shule ya msingi Ilungu anayetuhumiwa kuwadhalilisha kingono na kuwafanyia michezo michafu wanafunzi wawili kwenye kitanda kimoja kwa muda wa miaka saba kuondolewa Wilayani humo.

Agizo hilo amelitoa kwenye kongamano la kuweka mikakati ya kukabiliana na ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mimba na ndoa za umri mdogo, utoro kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu na ndipo alipotoa maelekezo hayo.

“Kesi ambazo tulizibaini ikiwepo Mwalimu mmoja anayeitwa Mambosasa tulimkamata akiwa na mahusiano na wanafunzi zaidi ya watatu, na wakati mwingine alikuwa anawalaza kwenye kitanda kimoja wote wawili na kuwafanyia mambo ya ajabu sana, nimesema mimi simtaki kwenye wilaya yangu” DC Kalii.

“MNATUHARIBIA KAZI” WAZIRI MKUU ATINGA BANDARINI, AWABANA MADEREVA, ATOA MAAGIZO KWA MABOSS

Chanzo: millardayo.com