Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu atoweka, akutwa amefariki kwenye mashamba ya miwa

Auawa Mwalimu INATISHA: Mwalimu atoweka, akutwa amefariki kwenye mashamba ya miwa

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: Wasafifm

Lightness Peter (29) mwalimu katika moja ya shule binafsi ya awali iliyopo katika eneo la Shabaha wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa katika mashamba ya miwa ya TPC yaliyopo nje kidogo ya mji.

Lightness alipotea tangu tarehe 20 julai mwaka huu ambapo juhudi za kumtafuta ziliendelea ikiwa ni pamoja na kutolewa matangazo katika vyombo vya habari bila mafanikio yeyote, jambo lililopelekea wazazi wake kukata tamaa ya kumtafuta.

Aidha Jana majira ya saa 6 za mchana walinzi wa mashamba hayo ya TPC waliona kundi kubwa la mbwa wakiwa wamejikusanya jambo lililowafanya kufuatilia nini kipo katika eneo hilo, ambapo baadae walikuta mabaki ya mwili huo, na kuwashirikisha majirani wa eneo hilo ambao walitambua nguo za lightness na vitu kadhaa vilivyokuwemo kwenye pochi yake.

Chanzo: Wasafifm