Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu anayedaiwa kulawiti, kubaka wanafunzi afikishwa Mahakamani

Mbaroniiiiiiiii Mwalimu anayedaiwa kulawiti, kubaka wanafunzi afikishwa Mahakamani

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu wa Shule ya Msingi Global International School iliyopo Mtaa wa Vijana, Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chacha Magere (26), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kubaka, kuwalawiti na kuwashambulia kwa aibu baadhi ya wanafunzi wake anaowafundisha.

Jumla amesomewa mashtaka sita.

Mwendesha Mashtaka wa Wakili wa Serikali, Hilda Kato ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Frankoo Kiswaga kuwa mtuhumiwa kwa nyakati tofauti Januari na Mei 2022 akiwa shuleni kwake aliwabaka na kulawiti wanafunzi wake wa kike (majina yamehifadhiwa) kinyume na sheria.

Aidha, Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali Daisy Makalala amedai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Aron Lyamuya kuwa mtuhumiwa akiwa kazini kwake alimlazimisha mwanafunzi wake wa kike kumnyonya sehemu zake za siri kwa lengo kujiridhisha kingono.

Shtaka lingine ni kumdhalilisha kingono mwanafunzi wake ambapo Mwendesha Mashtaka Daisy Makalala amedai katika tarehe hizo Mwalimu huyo mkazi wa Mwananyamala A akiwa shuleni kwake aliviingiza vidole vyake sehemu za siri za mwanafunzi wake wa kike (Jina linahifadhiwa) kwa lengo la kujiridhisha kingono.

Mtuhumiwa amekana tuhuma zinazomkabili na amepelekwa rumande baada ya upande wa mashitaka kuweka kiapo cha kupinga dhamana.

Upelelezi wa kesi hizo umekamilika na kuahirishwa mpaka Juni 13, 2022 ambapo yataanza kusomwa maelezo ya awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live