Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu ampa mimba mwanafunzi, DC acharuka!

DC MISS Mwalimu ampa mimba mwanafunzi, DC acharuka!

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Eatv

Watumishi katika Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, wametakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma na kuzingatia nidhamu kazini, ili kujijengea heshima kwa jamii wanayoiongoza. 

Hayo yamesema Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Wilson Sakulo, na kusisitiza kuwa nidhamu ni muhimu katika uwajibikaji.

"Kwa mfano mwalimu sehemu aliyopo ni kioo kwa wale wanafunzi anaowafundisha, haileti afya kuona huyo mwalimu ndiye anakuwa mstari wa mbele kuangalia zile sketi zilizoko pale shuleni, nimeona kuna changamoto za namna hiyo zimekuwa zikitokea, mfano kuna mwalimu hapa amempa mimba mwanafunzi na amekimbia," amesema Kanali Sakulo. 

Baadhi ya watumishi walioshiriki mafunzo hayo yanayolenga kuimarisha utendaji wao wa kazi, wamesema kuwa yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu hasa kwa watumishi wanaotoka vyuoni ambao hawajawa na uzoefu.

Chanzo: Eatv