Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu akamatwa na silaha ya kivita, nyara za Serikali

61317 Pic+mwalimu

Tue, 4 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Polisi mkoani Arusha limemkamata Mwalimu wa shule ya msingi Naan iliyopo Kata ya Enguserosambu tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro, Solomon Kipuker (30)  kwa kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali ikiwemo meno ya tembo, pembe, Faru na shughuli za ujangili kwa ujumla. 

Mwalimu huyo pia alikamatwa na silaha  ya kivita aina ya AK 47 pamoja na risasi tano zilizokuwa kwenye magazine.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Juni 4, 2019 Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna amesema polisi kwa kushirikiana na kikosi kazi kabambe dhidi ya ujangili na uhalifu wa silaha za moto kanda ya ziwa chini ya uwezeshwaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) walifanikiwa kumkata mshtakiwa huyo juzi Jumapili June 2, 2019.

Amesema baada ya kumhoji mshtakiwa huyo alikiri kumiliki silaha hiyo ya kivita kwa kushirikiana na watuhumiwa wengine ambao bado wanatafutwa.

Kamanda huo amesema silaha hizo zimekuwa zikitumika katika mapigano ya kikabila baina ya jamii ya Wasonjo na watemi na Wamasai na zimekuwa zikikodishwa katika matukio mbalimbali ya ujambazi na utekaji wa watalii, wananchi na mali zao.

Amesema mbali na tukio hilo katika kijiji cha Mbukeni Kata ya Arashi tarafa ya Loliondo silaha nyingine aina ya AK 47 ikiwa na risasi moja ilitelekezwa katika ofisi ya kijiji hicho baada ya taarifa za kiintelijensia kubaini uwepo wa bunduki hizo na washtakiwa hao wanatafutwa na polisi.

Pia Soma

Hata hivyo, jeshi hilo limefanikiwa kukamata majangili sugu hatari  watatu majina yao yamehifadhiwa wakiwa na nyara za Serikali Mei 30, 2019 katika kitongoji cha maji ya chai Kata ya maji ya chai na tarafa ya King'ori wilayani Arumeru .

Kamanda Shanna amesema watuhumiwa hao walipohojiwa na jeshi la polisi walikiri kuhusika na biashara hiyo na kukutwa wakiwa na vipande vinne vya meno ya Tembo walivyo kuwa wamehifadhi kwenye mfuko wa sandarusi na pindi upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha katika tukio lingine, polisi mkoani humo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wa wizi wa pikipiki ambao ni Hamis Juma (37) mkazi wa Olmatejoo, Isiaka Islamu (22) mkazi wa Majengo, Moshi  na Hassan Mushi (54) mkazi wa Majengo, Moshi ambao kwa pamoja walikutwa na pikipiki nne ambayo hutumika katika matukio ya wizi.

Kamanda Shana ametaja pikipiki hizo kuwa ni namba MC 978 CAH aina ya Haojue, MC 559 BHT aina ya Toyo, MC 427 BKP aina ya Boxer, na MC 789 BMC aina ya Boxer ambapo watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na jeshi hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz