Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu afungwa maisha kwa ulawiti, azimia mahakamani Dar

Aliyezuimia Pic Data Mwalimu afungwa maisha kwa ulawiti, azimia mahakamani Dar

Wed, 21 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Mwalimu wa Shule ya Kimataifa ya Global, Daniel Chacha, jana alianguka na kuzimia kizimbani, baada ya kutiwa hatiani na kuhukmiwa kifungo cha maisha jela kwa tuhuma ya kumlawiti mwanafunzi wake wa kike mwenye umri wa miaka sita.

Chacha ( 26) alipatikana na hatia katika mashtaka mawili kati ya matatu yaliyokuwa yakimkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Alikuwa akikabiliwa na shtaka la kubaka, kulawiti na kumfanyia shambulio la aibu mwanafunzi wake huyo.

Hata hivyo, katika Hakimu Mkazi, Aaron Lyamuya baada ya kusikiliza ushahidi na utetezi, alimtia hatiani kwa mashtaka mawili- shtaka la kulawiti na la shambulio la aibu.

Baada ya kumtia hatiani, Hakimu Lyamuya alimuuliza mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali, Daisy Makalala kama kuna kumbukumbu zozote za mshatakiwa kutiwa hatiani kwa makosa mengine yoyote ya jinai.

Wakili Makalala alijibu kuwa upande wa mashhtaka hawana kumbukumbu za makosa mengine ya mshtakiwa, lakini akaiomba mahakama hiyo impe mshtakiwa adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine.

Advertisement Kisha Hakimu Lyamuya alimpa nafasi mshtakiwa kujitetea kama ana sababu yoyote ya kumshawishi, lakini licha ya kumuuliza mara tatu, mshtakiwa hakujibu chochote bali aliendelea kukaa kimya ndipo hakimu Lyamuya akamtamkia adhabu hiyo.

“Sawa, hata kama ukikaa kimya sishangai maana adhabu hii iko kwenye sheria. Hivyo nakuadhibu kama ifuatavyo...,” alisema hakimu Lyamuya ya kuanza kutamka adhabu kwa kila kosa.

Alisema kuwa kwa kosa la kulawiti adhabu yake huwa ni kifungo cha maisha jela chini ya kifungu cha 154 (1) na (2) ya Sheria ya Kanuni za Adabu.

“Kwa kosa la tatu, sheria inatoa nafasi ya kupunguza adhabu lakini binafasi kwa jinsi nilivyokerwa na vitendo vyako ninakuhukumu adhabu ya juu kabisa ya miaka 30 jela. Kwa hiyo utatumia jela maisha yako yote yaliyosalia. Unayo haki ya kukata rufaa kama hujaridhika.”

Baada ya Hakimu Lyamuya kutamka adhabu hiyo askari magereza walimfuata mfungwa huyo kizimbani ili kumchukua kumpeleka gerezani kwa ajili ya kuanza maisha yake rasmi ya adhabu.

Hata hivyo, kabla askari hao hawajamfikia alidondoka kizimbani na kupoteza fahamu, hivyo ikawalazimu askari Magereza kumtoa mahakamani wakiwa wamembeba.

Mama wa mtoto huyo aliyefanyiwa ukatili huo, huku akilia alieleza kuridhishwa na hukumu hiyo akisema kuwa Mungu amejibu maombi yake na mshtakiwa amepewa alichostahili.

Mbali ya hukumu hiyo, mwalimu huyo bado anakabiliwa na kesi nyingine tatu kama hizo za kuwabaka na kuwalawiti wanafunzi wake.

Kesi hizo zipo katika hatua ya usikilizaji mahakamani.

Chanzo: Mwananchi