Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu afikishwa kortini kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake wa darasa la tano

Ubakaji Dhamana Mwalimu afikishwa kortini kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake wa darasa la tano

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, litampandisha Mahakamani wakati wowote, Mwalimu skuli ya Msingi ya Madungu wilaya ya Chake chake Pemba, Ali Makame Khatib, akidaiwa kumchezea sehemu zake za siri na kisha kumbaka, mwanafunzi wake wa darasa la tano skuli hapo.

Taarifa za Jeshi hilo, zilizotolewa na Kamanda wa Jeshi hilo mkoani humo, Abdalla Hussein Mussa alisema, kwa sasa wanaendelea kumuhoji mwalimu huyo, kuhusiana na tuhuma zinazomkabili, na kisha taratibu zikikamalika atafikishwa mahakamani.

Alieleza kuwa, awali walipokea taarifa za malalamiko kutoka kwa mama mzazi wa mtoto huyo, akidai mtoto wake, amechezewa na kisha kuingiliwa na mwalimu wake.

Kamanda huyo alieleza kuwa, baadae taratibu za kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, zilifuata na kuanza kuhojiwa juu ya tuhuma hizo.

Awali mama mzazi alidai kuwa, aligundua tatizo hilo kwa mtoto wake, baada ya kusikiliza moja ya kituo cha redio kikielezea aina za udhalilishaji.

Mama huyo alieleza kuwa, mtoto wake alimuambia kuwa, kama ni hivyo mwalimu wake, amekuwa akimchezea sehemu zake wakati anapotaka kumuadabisha akiwa skuli na wakati mwengine kumvua nguo yake ya ndani.

''Baada ya kuniambia hivyo, nilikwenda kituo cha Polisi Madungu wilaya ya Chake chake, na kutoa taarifa na kisha kukabidhwa fomu maalum ya 'PF3' na kwenda nayo kituo cha Mkono kwa mkono hospitali ya Chake chake,''alieleza.

Kisha mama huyo alirudi kituo cha Polisi Madungu na ndipo mwalimu huyo (mtuhumiwa) alipokamatwa na kuanza kuhojiwa.

Baadhi ya wananchi waliokataa kutaja majina yao, walisema mwalimu huyo amekuwa na tabia hiyo, na ndio maana amekuwa akihamishwa kutoka skuli moja kwenda nyingine.

Walisema wamekuwa wakimfuatilia mwalimu huyo, kutokana na vitendo vyake, ingawa hawakuwa wakipata ushahidi kamili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live