Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu afariki kwa kujinyonga

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza.  Mwalimu mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Bulale, Said Ngasa amefariki dunia kwa kujinyonga akiwa nyumbani kwake mtaa wa Nyambiti jijini Mwanza.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Paschal Faustine  ameiambia Mwananchi leo Jumanne Machi 19, 2019 kuwa tukio hilo lilitokea jana mchana.

"Sikuwepo shuleni wakati tukio lilipogundulika kwa sababu nilikuwa nahudhuria semina ofisi za jiji.”

“Nilipofika shuleni nilikuta mwili wa marehemu umeshachukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi," amesema Mwalimu Faustine.

Mwalimu Faustine amesema marehemu Ngasa alikuwa mcheshi, mwenye kujituma na juhudi katika kila kazi aliyokabidhiwa na alibakisha muda mfupi wa kastaafu.

Juhudi za kumpata kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Jumanne Muliro ambaye yuko kwenye ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzungumzia tukio hilo zinaendelea.



Chanzo: mwananchi.co.tz