Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakabibi na wenzake wamefikishwa Mahakamani

Mwakabibi Mahakm Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Lusubilo Joel Mwakabibi na mwenzake Edward Simon Haule ambaye alikuwa Mratibu wa Mradi wa DMDP wamewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo leo kesi inatarajiwa kutajwa.

Watuhumiwa hao walifikishwa Mahakamani Agosti 20 mwaka 2021, ikiwa ni agizo lililotolewa na Waziri Mkuu mara baada ya kutoridhishwa na utendaji katika miradi ya Maendeleo ya Wilayini humo ikiwa ni pamoja na ubadhilifu mkubwa wa fedha alio ubaini.

Hata hivyo, Mwakabibi na wenzake walisimamishwa kazi na Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu, Aprili 25, mwaka 2021 kufuatia kukithiri kwa malalamiko juu ya mwenendo usiofaa, matumizi mabaya ya madaraka na mwenendo usioridhisha wa usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live