Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakabibi, Mratibu wa Mradi DMDP Marufuku kutoka nje ya nchi bila kibali

IMG 2268 Scaled?fit=2560%2C1707&ssl=1 Mwakabibi, Mratibu wa Mradi DMDP

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusibilo  Mwakabibi na na Mkurugenzi na Mratibu wa  Mradi wa DMDP,  Edward   Haule wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na matumizi mabaya ya utumishi.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi, Ester Martin mbele Ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Evodia Kyaruzi imedai washtakiwa wametenda kosa hilo kati ya Machi  2020 na Machi 2021 katika Mkoa wa Dar  es Salaam.



Katika shtaka la matumizi mabaya ya madaraka imedaiwa, katika kipindi hicho, mshtakiwa Mwakabibi akiwa ameajiriwa Kama Mkurugenzi na Mratibu wa mradi wa DMDP walitekeleza  ujenzi  wa kituo cha basi cha Buza katika Kiwanja Kilichopo  buza kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana bila ruhusa kutoka kwa wamiliki.

Katika shtaka la Matumizi mabaya ya  ofisi  inadaiwa washtakiwa hao wakiwa waajiriwa wa Manispaa Ya Temeke Kama Mkurugenzi na Mratibu wa  Mradi wa DMDP  kwa maksudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kwenda kinyume na sheria ya Ardhi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na upande wa utetezi umeiomba mahakama itumie kifungu cha 29 (4) cha sheria ya Uhujumu Uchumi Ili kuwapa dhamana washtakiwa kwa kuwa mashtaka waliyosomewa  hayajataja Kiwango cha chochote cha fedha.

WAmeiomba pia Mahakama  kuweka  masharti nafuu ya dhamana yatakayowasiadia washtakiwa kufika mahakamani kila terehe itakayopangwa.

Hata hivyo, upande wa mashataka umedai kuwa hauna pingamizi ya dhamana lakini washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa shtaka linalowakabili ni la uhujumu uchumi.

Masharti ya dhamana washtakiwa wametakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh. Mil Kumi  ama hati ya mali  isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha pesa na kutotoka nje ya nchi bila Kibali na kesi imeahirishwa hadi Septemba 2,mwaka huu.

Chanzo: globalpublishers.co.tz