Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvuvi kortini akidaiwa kuiba kilo 27 za samaki

Hukumu Pc Data Mvuvi kortini akidaiwa kuiba kilo 27 za samaki

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvuvi, Athuman Salum (38) amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka la wizi wa kilo 27 za samaki zenye thamani ya Sh 350,000.

Salum, mkazi wa Mbagala, amefikishwa mahakamani hapo jana Januari 17, 2024 na kusomewa kesi na karani wa mahakama hiyo, Caroline Nyoni mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Clauds Kipande.

Karani Nyoni amedai mshtakiwa ametenda kosa hilo Januari 13, 2024, katika Soko la Samaki la Ferry lililopo Wilaya ya Ilala.

New Content Item (1)

Inadaiwa siku ya tukio saa 12 jioni, mshtakiwa aliiba kilo 27 za samaki, mali ya Hamisi Swalehe. Mshtakiwa amekana tuhuma hizo na kuomba Mahakama impe dhamana.

Hakimu Kipande baada ya kusikiliza kesi hiyo ameiahirisha hadi Februari 5, 2024 itakapoitwa. Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada kutimiza masharti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live