Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muuguzi kortini kwa kuomba rushwa

2c96baab92a83fbd4e24c0fae8ccee71 Muuguzi kortini kwa kuomba rushwa

Mon, 30 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Wallace Kazili (52) kwa mashtaka ya kuomba rushwa ya Sh 200,000 toka kwa mgonjwa.

Mwendesha Mashitaka wa Takukuru Wilaya ya Igunga, Mazengo Joseph aliiambia mahakama mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Igunga, Lydia Ilunda kuwa mshitakiwa Kazili anayeishi mtaa wa Masanga katika kata ya Igunga, alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 15(1)(a)na(2) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa No. 11, 2007.

Mazengo aliiambia mahakama kuwa Oktoba 30, mwaka huu, mshitakiwa Kazili akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga kama muuguzi aliomba rushwa ya Sh 200,000 kutoka kwa Kasembe Nangale mkazi wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga ili aweze kumpatia dawa ya Kifua Kikuu (TB) Bugumba Lisawi ambaye alikuwa amelazwa Hospitali ya Wilaya Igunga.

Alisema katika tarehe hiyo mwezi huo mshitakiwa Kazili alipokea 50,000 kwa njia ya simu kama malipo ya awali ya Sh 200,000 alizoomba.

Alisema Novemba mosi mwaka huu mshitakiwa huyo alipokea Sh 50,000 tena kama malipo mengine ya awali ya Sh 200,000 na kufanya kupokea jumla ya Sh 100,000 kati ya Sh 200,000.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 10, 2020 itakapoanza kusikilizwa na mshitakiwa yupo nje kwa dhamana ya Sh 300,000.

Chanzo: habarileo.co.tz