Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muuguzi kizimbani kwa kumlawiti msichana hospitalini

Mahakama Mahakama Muuguzi kizimbani kwa kumlawiti msichana hospitalini

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muuguzi wa Zahanati ya Saint Theresia wilayani hapa, Joseph Kiungi (25) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya akituhumiwa kumlawiti binti wa kidato cha pili (jina limehifadhiwa).

Akimsomea mashitaka hayo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Mazoya Luchagula mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, James Mhanus alisema Kiungi alitenda kosa hilo Oktoba 13 akiwa katika zahanati hiyo ambako binti huyo alikwenda kutibiwa.

Hata hivyo, Kiungi alikana mashtaka hayo. Mwendesha mashtaka alisema upelezi wa shauri hilo umekamilika na anao mashahidi wanne na kuiomba mahakama isome maelezo ya kosa ili ianze kusikilizwa.

Akitoa ushahidi huku akibubujikwa machozi, binti aliyefanyiwa ukatili huo aliieleza mahakama kuwa Oktoba 13 alikwenda katika Zahanati ya Saint Theresia kuchoma sindano ya tetenasi na alipokelewa na muuguzi huyo aliyemwelekeza kwenda chumba cha sindano.

Alisema muuguzi huyo alimwambia atampa kidonge na sindano kisha wakaongozana hadi chumba cha sindano.

Binti huyo alisema walipofika chumbani humo, muuguzi huyo alimwambia avue nguo za ndani na ainame kwa kuwa kuna kidonge anataka kumwekea sehemu ya haja kubwa ndipo amchome sindano na yeye alitekeleza maelekezo aliyopewa.

Alisema baada ya kuinama alihisi maumivu makali sehemu ya haja kubwa ndipo akainuka na kugeuka nyuma na kumwona mshtakiwa akiwa ameshusha suruali yake huku uume wake akiwa ameuweka kwenye sehemu yake ya haja kubwa hivyo akapiga yowe la kuomba msaada.

Huku akiomba msaada huo, alisema alikimbi akutoka chumba hicho cha sindano na alipofika eneo la mapokezi katika zahanati hiyo, aliomba simu ili awapigie wazazi wake lakini wauguzi waliokuwa mapokezi walimwambia amsubirie daktari mkuu wa zahanati hiyo jambo ambalo hakuliafiki hivyo akaazima simu kwa mmoja wa wagonjwa waliokuwepo katika zahanati hiyo na kumpigia baba yake kumweleza kila kitu kilichomtokea.

Baada ya baba yake kupata taarifa hizo, alisema alifunga safari na alipofika katika zahanati hiyo alimkuta binti hivyo wakapiga simu kituo cha polisi na maofisa wa jeshi hilo waliwasili katika zahanati hiyo na kumkamata mshtakiwa waliyeongozana naye mpaka kituoni kwa ajili ya utaratibu mwingine wa kisheria.

Binti mwenyewe pia alisema alienda kutoa maelezo kituo cha polisi na kupewa fomu namba 3 (PF3) ambayo aliyoenda nayo Hospitali ya Wilaya Chunya na kufanyiwa vipimo vya kitaalamu kuthibitisha tendo alilofanyiwa n a muuguzi huyo kisha kurudi nyumbani.

Baada ya binti huyo kumaliza kutoa ushahidi wake, mwendesha mashtaka alisema hawana pingamizi la dhamana hivyo mshitakiwa alitakiwa kuleta wadhamini wawili watakaosaini hati ya Sh10 milioni kila mmoja pamoja na mshtakiwa mwenyewe.

Hata hivyo, mshtakiwa alirudishwa mahabusu kwa kishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo kuhairishwa mpaka Oktoba 18 itakapoitwa tenakwa ajili ya kusikiliza mashahidi wengine waliobaki kabla ya kumruhusu mshtakiwa kujitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili na kumruhusu hakimu kuamua haki ya kila upande katika tuhuma hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live