Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muuguzi anayedaiwa kumpiga mjamzito asimamishwa kazi

E8110127278c0a9144e7537226782f26 Muuguzi anayedaiwa kumpiga mjamzito asimamishwa kazi

Wed, 13 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI Mtendaji wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Jacob Mtalitinya amemsimamisha kazi muuguzi Valencine Kinyanga akituhumiwa kumtolea lugha chafu na kumshambulia kwa kumpiga makofi mjamzito aliyejifungua sakafuni wakati akisubiri kuhudumiwa katika wodi ya wazazi.

Inadaiwa kuwa Kinyanga alifanya vitendo hivyo usiku wa manane Januari 10 katika wodi ya wazazi kwenye kituo cha afya cha Mazwi mjini Sumbawanga.

Katika siku ya tukio Kinyanga alikuwa muuguzi wa zamu. "Ni kweli kisa hicho kimetokea katika kituo cha afya Mazwi...hatua ya awali niliyochukua dhidi ya muuguzi huyo nimemsimamisha kazi kupisha uchunguzi wa shauri lake "alisema Mtalitinya.

Taarifa kutoka kituoni hapo zinadai kuwa, mjamzito huyo (jina limehifadhiwa) aliripoti kituoni hapo Januari 10 saa saba usiku na alizingatia taratibu zote.

Mashuhuda wa mkasa huo kwa masharti ya kutoandikwa gazetini walidai kuwa muuguzi wa zamu, Kinyanga, alimpokea mjamzito huyo na kumpeleka katika wodi ya wazazi akisubiri kujifungua.

Inadaiwa kuwa muuguzi huyo baada ya kumfikisha mjamzito huyo wodini aliondoka na kuendelea na shughuli zingine kituoni hapo.

"Mjamzito huyo alianza kuhisi maumivu makali ya uzazi alipiga kelele kuomba msaada ndipo muuguzi wa zamu (Kinyanga) alitokea na kumsihi aendelee kusubiri... muuguzi huyo aliondoka tena" alidai mmoja wa mashuhuda.

Inadaiwa kuwa uchungu wa uzazi ulipomzidi mjamzito huyo alitandika kanga zake sakafuni na kujifungua kitendo kilichomuudhi muuguzi huyo wa zamu..

Inadaiwa kabla muuguzi huyo wa zamu kuingia wodini humo, wajawazito waliokuwa wakisubiri kujifungua walimsaidia mwenzao huku wakipiga kelele wakiomba msaada.

"Muuguzi huyo wa zamu alipoingia wodi na kushuhudia mjamzito huyo amejifungua sakafuni alihamaki na kuanza kumfokea huku akimzaba makofi "alidai mtoaji taarifa.

Aliendelea kudai kuwa, baadaye muuguzi huyo alimsaidia mama huyo ambaye mtoto aliyejifungua anaelezwa kubwa na siha njema.

Chanzo: habarileo.co.tz