Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muuaji wa Shinzo Abe ahamishwa chap!

MAUAJI ONE TWO Muuaji wa Shinzo Abe ahamishwa chap!

Tue, 12 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshukiwa wa mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe alihamishwa baada ya kuhifadhiwa kwenye kituo cha polisi kwa siku mbili, Julai 10, 2022.

Mshukiwa huyo alikamatwa na polisi mara moja baada ya tukio hilo la mauaji kutokea, mshukiwa huyo alifahamika kwa jina la Tetsuya Yamagami mwenye umri wa miaka 41, mwanachama wa zamani wa Kikosi cha Kujilinda cha nchi hiyo.

Polisi wanasema mshukiwa aliamini kwamba Shinzo Abe ni sehemu ya kikundi cha kidini ambacho hakijabainishwa alichokilaumu kwa kusababisha anguko la kiuchumi au kufilisika kwa mama yake, Ingawa amesema alikusudia kumuua Abe, anasisitiza kuwa nia yake haikuwa ya kisiasa, kulingana na polisi.

Yamagami alitumia bunduki ya kujitengenezea nyumbani katika ufyatuaji risasi ambapo polisi walipata silaha zaidi kama hizo nyumbani kwake, aliwaambia polisi kwamba alitengeneza bunduki kwa kufunga mabomba ya chuma pamoja na mkanda, kulingana na NHK.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live