Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muuaji maarufu Njombe 'Mtoa Roho' akamatwa

Auwawapic Data Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Khamis Issah

Fri, 4 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Mkoa wa Njombe wanawashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za mauaji yanayodaiwa kufanyika katika matukio tofauti ndani ya mkoa huo.

Kamanda wa Polisi Khamis Issah amewataja kwa majina waliouawa ni Susana Mtitu na Kassim Kitamkanga ambao miili yao ilikutwa imetupwa katika msitu wa Tanwat Njombe mjini, Haskari Msigwa mtoto wa miaka saba na mwanafunzi wa awali shule ya msingi kilima hewa aliyeuawa na baba yake mzazi kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili na waya na Mesia Kaduma mtoto wa miaka mitano mwanafunzi wa awali shule ya msingi Kaduma huko wilayani wangingombe.

Katika matukio hayo Polisi Mkoa wa njombe Inawashikilia watu kadhaa kwa tuhuma hizo akiwemo Joseph Mgunda ambae ni Mganga wa Jadi na Endrew Varuhoka wanaodaiwa kutekeleza mauaji ya Suzan Mtitu na Kassim Kitamkanga.

Aidha Polisi wanamshikilia Izrael Msigwa Maarufu kwa Jina la #MtoaRoho anayedaiwa kutekeleza mauaji ya mtoto wake Haskar Izrael Msigwa kwa kumpiga mtoto huyo akitumia waya kwa madai ya kujisaidia haja ndogo kitandani.

Pia polisi wanawashikilia Ambwene Sanga (34) na Michael Mbilinyi (32) kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Mesia Kaduma aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya maingi katika wilaya ya Wanging'ombe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live