Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muongoza watalii atupwa jela miaka mitatu kuomba rushwa

Migration Olakira Lamai Safari Traveller 9jul13 Pr Muongoza watalii atupwa jela miaka mitatu kuomba rushwa

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa, Agosti 24, 2022 imefungua shauri la jinai Na. CC. 95/2022 dhidi ya Elisha Christopher Mashamba ambaye ni muongoza watalii katika hifadhi ya misitu ya Tongwe East - Nkondwe Waterfalls Camp.

Mashamba alikuwa akishitakiwa kwa tuhuma za kuomba na kushawishi rushwa ya Tsh. 50,000.

Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Gway Sumaye na katika kesi hiyo mshtakiwa amekiri makosa yake na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Tsh. 500,000.

Aidha, mshitakiwa ameomba kulipa faini na kupelekwa gerezani kwa maelekezo ya hakimu kuwa ndugu zake watakapoleta hiyo faini atatolewa gerezani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live