Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume, mke mbaroni kwa madai ya kuua mtoto wao

62892 MAUAJI+PIC

Sun, 16 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Jeshi la Polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wawili ambao ni mume na mke kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mtoto wao wakidaiwa kumchuna ngozi kwenye paji la uso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire alisema tukio hilo lilitokea jana saa sita machana katika Kijiji cha Kinegembasi, Kata ya Kitandula Tarafa ya Kisanga Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Kamanda Bwire aliwataja wazazi wa mtoto huyo kuwa ni Patson Kitangwila (27) mkewe Neema Nzilo (31) ambao wote ni wakulima wa Kinegembasi.

Kamanda Bwire alisema mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Laurent Kitangwila alikuwa na umri wa miezi miwili na alikufa akiwa amelala na wazazi wake usiku ambao walipoamka walimkuta akiwa na jeraha la kuchunwa ngozi katika paji la uso.

“Mtoto huyu akiwa amelala na wazazi wake wote wawili, wameamka asubuhi wakakuta amekatwa na kitu chenye ncha kali ambacho kilimchuna ngozi kwenye paji la uso hadi puani na kufariki lakini wamekuja kutoa taarifa saa sita mchana. Tumewakamata wazazi wote wawili na tunaendelea na uchunguzi,” alisema Bwire.

Kamanda Bwire alisema kwamba katika ukaguzi wa tukio hilo, jengo na nyumba walimokuwa wamelala hapakuwa na sehemu yoyote iliyovunjwa wala dirisha lililovunjwa na kwamba, “kila kitu kilikuwa kipo sawa, cha ajabu hakuna damu yoyote pale alipokuwa amekatwa au pale alipolala kitandani na ndio maana wazazi nao wameshikiliwa kuisaidia polisi.”

Pia Soma

Kamanda Bwire alisema baada ya mahojiano ya awali inasemekana baba wa mtoto usiku ule alitoka na mtoto akaenda sehemu isiyojulikana.

Alisema jeshi hilo linaendelea kufuatilia na limewakamata watu watano wakiwamo waganga wa kienyeji wawili na wanaendelea kuchunguza sababu ya tukio hilo alilosema linawapa utata na hawajajua chanzo cha mtoto huyo kujeruhiwa kwa njia za namna hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz