Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume, mke kortini tuhuma za kusafirisha meno ya tembo ya bil 4.4/-

460258fa4a6778a5c8aec3fd926de08c Mume, mke kortini tuhuma za kusafirisha meno ya tembo ya bil 4.4/-

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Chamazi Wilaya ya Temeke, Abdul Abdallah (35) na mkewe, Salama Mshamu (21) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwamo la kununua na kusafirisha nyara za serikali bila kibali.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Timotheo Mmari akiwa na Wakili wa Serikali, Mosie Kaima alisoma mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Pamela Mazengo.

Mmari alidai kuwa kati ya Julai Mosi, 2017 na Septemba 3, 2019 katika eneo la Chamazi Saku, Abdul na Salama walikubali kupokea, kununua na kusafirisha vipande 413 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh bilioni 4.4.

Katika shitaka la pili inadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi 2017 na Septemba 3, 2019 katika eneo hilo hilo, washitakiwa walikutwa na meno mawili ya mnyama aina ya kiboko yenye thamani ya Sh 3,452,000 bila ya kuwa na kibali kinachowaruhusu kumiliki nyara hizo. Katika shitaka la mwisho wakili, Mmari alidai washitakiwa wote wawili katika tarehe tajwa na eneo tajwa walikutwa na nyara za serikali pasi na kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Wakili wa Serikali, Timotheo Mmari alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wanasubiri kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka ili kesi hiyo iweze kuendelea kwa hatua nyingine na kuiomba mahakama tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Wamerudishwa rumande hadi Agosti 2, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live