Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume atuhumiwa kumuua mkewe, polisi wamsaka

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Polisi mkoani Tabora linamtafuta mkazi wa kitongoji cha Ulanga B, wilayani Kaliua mkoani humo, Hamis Nepo kwa tuhuma za kumuua mkewe, Pendo Samora na kisha kukimbia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley akizungumza leo Jumanne Machi 19, 2019 amesema tukio hilo, limetokea jana Jumatatu saa tano na nusu asubuhi.

Kamanda Nley amesema mtuhumiwa alimpiga mkewe kwa fimbo kisogoni na kusababisha kifo chake.

Ameeleza chanzo ni ugomvi baina yao baada ya mwanaume kuuza pikipiki na pesa kutaka kuoa mke mwingine aitwaye, Monica Said anayeishi kijijini hapo.

Kamanda Nley amesema mara baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia na anatafutwa na polisi akihusishwa na mauaji hayo.



Chanzo: mwananchi.co.tz