Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume anyonga mke kwa wivu, naye ajinyonga

82924 Wivu+pic Mume anyonga mke kwa wivu, naye ajinyonga

Wed, 6 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga. Watu wawili, mume na mke wamefariki dunia katika matukio tofauti kwa mume kumnyonga hadi kufa mke wake kabla naye hajajitoa roho kwa kujinyonga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa matukio hayo yalitokea Novemba 3, 2019 katika Kijiji cha Mwanima wilayani Kishapu.

Alimtaja mwanamke aliyeuawa kwa kunyongwa shingo na mume wake kuwa ni Pendo Nela (20) mkazi wa Kijiji cha Mwanima wilayani Kishapu.

Alisema baada ya tukio hilo, mume aliyemtaja kwa jina la John Paul (27) alikimbilia kijiji jirani cha Mwakoloma wilayani Kishapu alikojinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua cha mbu na mwili wake kukutwa ukining’inia juu ya mti.

“Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha vifo hivyo ni wivu wa kimapenzi,” alisema Kamanda Abwao.

Alisema kabla ya vifo vyao, mume huyo John Paul alikuwa akimtuhumu mke wake Pendo Nela kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine. Kamanda Abwao aliwataka wananchi mkoani humo kuepuka tabia ya kujichukulia sheria mikononi, badala yake watumia mamlaka na njia sahihi kutatua changamoto na migogoro yao ambapo ile inayohusiana na ndoa akishauri wawashirikishe wazee wa mila, wazazi na viongozi wa dini.

Chanzo: mwananchi.co.tz