Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume amuua mkewe ukweni kwa kumchoma kisu

Kisuu Mume amuua mkewe ukweni kwa kumchoma kisu

Tue, 19 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia Seleman Malima almaarufu Jiwe, mkazi wa Goba kwa Awadhi, kinondoni kwa tuhuma za kumuua mkewe aliyefahamika kwa jina la Husna Majaliwa kwa kumchoma kisu.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Julai 12, 2022 ambao wawili hao walikuwa na ugomvi uliosababisha mwanamke arudi nyumbani kwao, ambapo mwanaume huyo alimfuata akidai amekwenda kumwona mtoto wake ambapo ndipo alipotekeleza tukio hilo.

"Mtuhumiwa alikwenda nyumbani kwa wazazi wa marehemu akidai amekwenda kumuona mtoto wake na wakati huo walikuwa na mgogoro wa kifamilia, wazazi waliwapa fursa ya kukaa nje na wakati wakiwa kwenye mazungumzo.

"Mtuhumiwa huyo alimchoma mke wake kwa kisu tumboni na baadaye akatoweka. Kitendo hicho kilisababisha kifo cha kifo cha mama huyo niliyemtaja kwa jina la Husna.

"Uchunguzi wa kina ulianza mara moja baada taarifa kufika kituo cha pilisi, ilipofika Julai 18, 2022 mtuhumiwa huyo alikamatwa katika jiji la Dodoma kwenye eneo linalofahamika kama Mbande na baadaye akarejeshwa jijini Dar es salaam.

"Mahojiano ya kina yalifanyika, na hatimaye mtuhumiwa huyo alionyesha kisu alichokitumia kumuua mke wake. Polisi inakamilisha uchunguzi wake ili mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria ikiwemo mahakama.

Aidha, Kamanda Muliro ametoa wito akiwataka watu wanaokuwa kwenye migogoro watumie taasisi mbalimbali za utatuzi wa migogoro ikiwemo taasisi za kidini, mabaraza mbalimbali na vyombo vingine vya serikali vyenye dhamana ya kusikiliza na kutatua migogoro mbalimbali ya kifamilia badala ya kuchukua hatua za kutenda au kufanya kmakosa ya jinai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live