Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume amuua mkewe kwa madai ya kuoteshwa na mganga kuwa ni mchawi

Kamanda Abwao Mume amuua mkewe kwa madai ya kuoteshwa na mganga kuwa ni mchawi

Tue, 20 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia Ali Idd Mkonongo, mkazi wa Kijiji cha Inala kwa tuhuma za kumuua mke wake aliyefahamika kwa jina la Mariam Yusuph kwa kumpiga na kitu kizito kichwani wakati akiwa amelala majira ya saa sita usiku, kisha kuuchukua mwili na kuudumbukiza kisimani kwa lengo la kupoteza ushahidi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao, mwanaume huyo alitekeleza mauaji hayo baada ya kutoka kupigiwa ramli kwa mganga wa kienyeji na kuelezwa kwamba atamuona mchawi wake ndotoni.

Baada ya kumuota mkewe, Ali amua kufanya mauaji hayo akitekeleza kile alichokiota ndotoni.

Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilisha taratibu za uchunguzi dhidi ya mauaji hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live