Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume amnyofoa jicho mkewe

Kisuu Mume amnyofoa jicho mkewe

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maureen Atieno Omollo; ni mwanamke ambaye ameibuka na kuelezea unyama aliofanyiwa na mumewe kwa kukatwa kidole, kunyofolewa jicho na kuchomwa na visu mwilini.

Mauree anasema kuwa, wazazi wake walifariki dunia akiwa na umri wa miaka 9 na yeye ndiye alikuwa mtoto mkubwa.

Anasema kuwa, akiwa na miaka 15 ilibidi akubali tu kuolewa kishingo upande ili mwanaume husika amsaidie yeye na wadogo zake.

Lakini tatizo kubwa ni wivu uliokithiri aliokuwa nao mwanaume husika akawa anaishia kufungiwa ndani na hakuruhusiwa hata kuwa karibu na marafiki maana mume husika alihofia Maureen anaweza kuchukuliwa na mwanaume mwingine.

Kwa mujibu wa Maureen, mara kadhaa mume akawa anamwambia nitakuua siku nikijua unanisaliti, ila alidhani ni wivu tu wa kawaida, akajipa moyo kuwa atabadilika. Miaka ilipita, wakazaa watoto wanne, ila mmoja alifariki dunia.

Baada ya muda, Maureen alimuomba mumewe afanye kazi ili amsaidie majukumu ambapo mumewe alikubali, jambo ambalo hakulitarajia.

Maureen alisema kuwa, alipata kazi za ndani jijini Nairobi kwa hiyo ilibidi awe anafika kuitembelea familia yake mara kwa mara, ila mumewe bado alisisitiza kuwa atamuua akijua anamsaliti.

Siku moja, Maureen alirudi kuiona familia yake, ila alipatwa na mshtuko kukuta mumewe ameleta mwanamke mwingine ndani kwao wakati yeye aliishi Nairobi kwa kujitunza asimsaliti mumewe.

Maureen akaona hatakiwi tena, akataka kurudi kazini, ila mumewe alimwambia abaki atamfukuza huyo mwanamke mwingine, ila Maureen alirudi alikotoka baadaye.

Siku hiyo, mumewe alimwambia Maureen usiporudi nawaua watoto tuliozaa, kusikia hivyo, Maureen akarudi, akawa wanaishi wote na huyo mke mwenza ingawa hakupikika chungu kimoja, ila waliishi hivyohivyo.

Maureen anasema alitaka kurudi Nairobi kudai pesa ambazo alikuwa bado hajalipwa na bosi wake, lakini mumewe anadhani ndiyo anaondoka moja kwa moja kwani hakutaka Maureen awe na mwanaume mwingine maishani la sivyo atamuua.

Baadaye, mumewe alimpigia simu ndugu wa kiume wa Maureen kumwambia anamuua na kabla ndugu hajamtaarifu Maureen akimbie tayari mume alimvamia Maureen na sime ambalo lililetwa na mke mwenza, akachomwa mwilini na kutolewa jicho.

Mumewe huyo alijisalimisha Polisi baada ya kudhani amemuua Maureen, lakini alitibiwa hospitalini na hivi sasa anauza vitu vidogovidogo kulea watoto wake. Anamalizia kwa kusema hajui yule mke mwenza alikimbilia wapi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live