Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume adaiwa kuua mke na kumtelekeza hospitali

574fd46d019710e1072a5f34151dde61 Mume adaiwa kuua mke na kumtelekeza hospitali

Thu, 21 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi mkoani Manyara linamtafuta mkazi wa kijiji cha Gidas, wilayani Babati, Doh Hamsii Kodi akituhumiwa kumpiga mkewe na kumsababishia kifo kutokana na wivu wa mapenzi.

Mwananchi huyo pia anatuhumiwa kumtelekeza mkewe hospitali wakati akiendelea kupata tiba kutokana na kipigo hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Paul Kasabago amemtaja marehemu kuwa ni Juliana Gadie (45) na kwamba, alipigwa na mumewe akimtuhumu kuwa hakuwa mwaminifu kwenye ndoa yao.

"Chanzo cha tukio hili ni wivu wa mapenzi kutokana na mume kwani mume alikuwa akimtuhumu mara kwa mara mke wake kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa ndipo alipoamua kumpiga na kitu butu kichwani hali iliyosababisha kupata maumivu makali." Alisema.

Kamanda Kasabago alisema mtuhumiwa alipoona mkewe amezidiwa alimpeleka zahanati ya kijiji cha Gidas ambako aliaga dunia kabla ya kupata matibabu.

"Mume wake ambaye ni mtuhumiwa alipobaini mke wake amefariki alichofanya ni kumwambia nesi ngoja niende hapo mnadani nikawaite ndugu wa marehemu kutokana na siku hiyo ilikuwa siku ya mnada wa Gidas na kuchukua bodaboda na kuondoka na hakurudi mpaka leo hivyo tunaendelea kumtafuta," alisema.

Alisema baada ya kufanya uchunguzi wataalamu wa hospitalini hapo waligundua pamoja na kupigwa na kitu kibutu kichwani, lakini pia mama huyo alinyongwa.

Kamanda Kasabago alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na serikali ya kijiji bado linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo ili aweze kufikishwa mahakamani.

Chanzo: habarileo.co.tz