Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume adaiwa kumuua Mkewe na kumchoma moto

7A2AA8FA D09E 4DA7 ADDB 96522F321D98.jpeg Mume adaiwa kumuua Mkewe na kumchoma moto

Wed, 19 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Ilanga kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe, Subira Kibona(16) amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni kisha mwili wake kuchomwa moto na anayesadikika kuwa mume wake, Shukrani Kamwela (16) kabla ya kutupa mabaki ya mwili huo kwenye korongo.

Kamada wa Jeshi la Polisi mkoani Songwe, ASP Janeth Magomi, akizungumzia tukio hilo, amesema walipokea taarifa za tukio hilo juu ya mwanamke huyo ambaye alipotea nyumbani tangu Januari 13, mwaka huu.

ASP Magomi amesema baada ya kutoonekana kwa marehemu huyo wananchi walifanya juhudi za kumtafuta ndipo walipokuta mwili wake ukiwa umetupwa katika korongo lililopo katika moja ya pori mkoani humo huku ukiwa umechomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya mgongoni na kuchomwa moto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live