Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume adaiwa kumkata mkewe masikio

81592 Maskio+pic Mume adaiwa kumkata mkewe masikio

Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mkami Mwitonyi, amelazwa hospitali ya Nyerere wilayani Serengeti akiuguza majeraha baada ya kukatwa masikio na mumewe.

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 24, 2019 mganga wa zamu  wa hospitali hiyo, John Mororo amethibitisha kumpokea majeruhi huyo mkazi wa kijiji cha Mesaga, kubainisha kuwa amekatwa katika masikio na kitu chenye ncha kali.

Amesema sehemu ya masikio yake mawili yamekatwa na wanaendelea kumpatia matibabu.

Akizungumzia tukio hilo, Mkami amesema simu ya mume wake ilipotea na yeye kuhisiwa kuwa ameificha, “alinifunga kamba na kunikata masikio alikuwa na lengo la kuniua na baada ya kufanya kitendo hiki alitokomea na kuniacha.”

Akizungumza na Mwananchi ofisa mtendaji kata ya Kenyamonta,  Saganda Bodo amedai mtuhumiwa alimnasa mke akizungumza na simu na mwanamke mwingine.

Amesema tukio hilo liliibua mvutano na mwanaume huyo kuamua kukata masikio ya mkewe kwa madai kuwa amekuwa hasikii kila anachomueleza.

Pia Soma

Advertisement
Amesema polisi wanashirikiana na uongozi wa kijiji kumsaka mtuhumiwa huyo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz