Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume adai hasira zilimpelekea kumuua mkewe

AMINA AFARIKI Mume adai hasira zilimpelekea kumuua mkewe

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Geita linamshikilia Mashaka Jeremia mkazi wa mtaa wa Mkoani, Halmashauri ya mji Geita kwa tuhuma za kumuua mke wake Amina Iddy (pichani) kwa kumchoma visu zaidi ya 10 mwilini na kusema alimuua sababu ya hasira baada ya kuuza shamba bila kumshirikisha.

Tukio hilo liliripotiwa Septemba 2, mwaka huu na Amina alichomwa visu hivyo usiku wa Agosti 30, 2022, na aliacha watoto wawili wa kike.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe, amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 6 wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera akijaribu kujificha baada ya kutekeleza tukio hilo.

"Tumemhoji, amekubali kuhusika na mauaji ya mke wake, akidai kwamba ni hasira, eti mke wake aliuza shamba bila kumshirikisha ndio akaaamua kufanya kitendo kama hicho, upelelezi wa shauri umekamilika kwa upande wa Polisi na mshtakiwa anafikishwa mahakamani leo kwa kosa la mauaji," amesema Kamanda Mwaibambe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live